Huajian Group yaonesha dhamira kuwekeza Tanzania

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule akiongozana na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Bw.Ally Gugu na Mkurugenzi wa Jiji, Bw.Joseph Mafuru siku ya Mei 11, 2023 wamepokea ugeni kutoka China ukiongozwa na Bw.HuaRong Zhang mmiliki wa Huajian Group akiwa na lengo la kuwekeza katika Kiwanda kikubwa cha kutengeza viatu nchini.

Mhe. Senyamule amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufungua fursa za uwekezaji nchi na amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia mazingira rafiki ya uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma.

Huajian Group ni miongoni mwa makampuni makubwa ndani na nje ya China iliyoanzishwa mwaka 1996 huku makao yake makuu yakiwa huko Dongguan China.

Wanajishughulisha na utengenezaji wa viatu vya ngozi vya wanawake vyenye ubora wa hali ya juu duniani. Aidha,wanamiliki vituo vitatu vikuu vya uzalishaji huko Dongguan,Ganzhou nchini, na Ethiopia barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news