Makamu wa Rais awasili jijini Bujumbura

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchoir Ndadaye uliopo Bujumbura nchini Burundi na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Burundi Mheshimiwa Prosper Banzombaza leo Mei 6, 2023.





Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika Bujumbura nchini Burundi.(Picha na OMR).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news