Mels Daalder apewa jukumu Simba SC

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa Klabu ya Simba umemteua Mels Daalder raia wa Uholanzi kuwa msaka vipaji (Skauti Mkuu) ambaye ana uzoefu wa kufanya skauti kwenye timu mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba SC, Mels ameshiriki kozi mbalimbali za duniani ikiwa ni pamoja na zilizoendeshwa na skauti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.

Mels ambaye ameshawahi kuishi Tanzania ni shabiki mkubwa wa Simba pia ni mjuzi wa kufanya upembuzi (analysis) na anaijua vizuri ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Pia, Mels anaongea lugha kadhaa ikiwemo Kiholanzi, Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili kwa kiasi fulani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema eneo la skauti ni muhimu ingawa lilikuwa halipewi nafasi kubwa na kwa kuliona hilo wameamua kumleta Mels.

"Tunafuraha kubwa kumkaribisha Mels ili kuja kuboresha ufanisi kwenye skauti kwakuwa ni eneo muhimu katika mafanikio ya klabu yetu. Tunaendelea na maboresho muhimu kuelekea msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa,”amesema Kajula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news