Musoma Vijijini waanza kujiandaa kwa taratibu za mazishi na maziko ya Mheshimiwa Nimrod Mkono

NA DIRAMAKINI.

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoani Mara Prof. Sospeter Muhongo amewaomba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Vijijini na wananchi wa Jimbo hilo kwa ujumla, kujitokeza kushiriki kikamilifu katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Butiama Nimrod Mkono kwa tarehe itakayopangwa ndani ya mwezi huu.
Prof.Muhongo ameyasema hayo kupitia taarifa yake aliyoitoa leo Mei 16, 2023. Ambapo maziko yatafanyika kijijini kwao Busegwe Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

"Ndugu zangu,ninaomba kuwataarifu kwamba maziko ya marehemu Mbunge wetu yatafanyika kijijini kwao Busegwe (Wilaya ya Butiama) ndani ya mwezi huu (tarehe tutajulishwa).

"Ninapenda kuwashawishi na kuwasihi TUSHIRIKI IPASAVYO, alikuwa Mbunge wetu kabla ya jimbo kugawanywa na kuzaa majimbo mawili (Musoma Vijijini na Butiama.
 
"Je, ni wangapi wangalipenda kuhudhuria maziko yake, kwa tarehe itakayopangwa na wafiwa? Ninaomba Kamati ya Siasa ya Wilaya yetu ipate orodha ya washiriki hao.Michango kutoka Musoma Vijijini, Kamati ya Siasa ya Wilaya yetu iweke utaratibu wa kupokea michango hiyo na kuiwasilisha kwenye Kamati ya Maziko ya Busegwe," amesema Prof.Muhongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news