OUT INAFUNDISHA UALIMU WALIMU WA UFUNDI

NA MWANDISHI WETU

CHUO Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa mafunzo ya ualimu kwa walimu wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kwa lengo la kuwajengea uwezo, na kuwapatia mbinu za ufundishaji na ujifunzaji walimu wa fani hii wakiwa wanaendelea na kazi zao.
Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Elifas Bisanda alipotembelea maonesho ya Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) tarehe 19/05/2023. Prof. Bisanda alisema kwamba:

"Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Ualimu wa Ufundi cha VETA Morogoro kinatoa program inayoitwa Postgraduate Diploma in Technical and Vocational Teacher Education (PGD-TVTE) kwa wahandisi wenye shahada ambao ni walimu katika vyuo vya ufundi. 


Programu hii ni nzuri sana kwani huwawezesha wahandisi na wengine wote wanafundisha katika vyuo vya ufundi kuwa na ujuzi wa mbinu za ufundishaji na ujifunzaji pamoja na ubunifu unaosadia kuzalisha mafundi wabobezi katika fani zao hapa nchini."

Prof. Bisanda alihitimisha kwa kutoa wito kwa wahandisi na watu wa fani nyingine ambao ni walimu wa ufundi au wanatarajia kuwa walimu wa fani za ufundi kujiunga na programu hii ambayo huwapatia fursa ya kusoma huku wakiwa wanaendelea na kazi zao popote pale walipo

Postgraduate Diploma in Technical and Vocational Teacher Education (PGD-TVTE) hufunzwa kwa mwaka mmoja wa masomo na maombi yanapokelewa kupitia www.out.ac.tz au fika kwenye kituo cha karibu cha OUT ujaze fomu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news