Prof.Bisanda atembelea Maonesho ya Pili ya NACTVET Arusha

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof.Elifas Bisanda amefanya ziara ya kutembelea Maonesho ya Pili ya Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Katika ziara hiyo Prof. Bisanda ametembelea banda la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambacho kinashiriki kwa mara ya pili katika maonyesho hayo. 

Pia, ametembelea vyuo na taasisi mbalimbali kuona zinavyojiimarisha katika kazi zao. Aidha, amefanikiwa pia kushudia uzinduzi wa maonesho hayo uliofanywa rasmi leo Mei 19, 2023 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda.
Maonesho ya pili ya Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), yalianza mnamo Mei 16, 2023 na yanatarajiwa kumalizika Mei 22, 2023 ambapo vyuo mbalimbali, taasisi na mashirika yaliyo chini ya baraza hilo yanashiriki kuonyesha umahiri wao kwa jamii katika kazi na utoaji wa huduma kwa jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news