Rais Dkt.Mwinyi aishukuru China kwa kuendelea kuunga mkono miradi ya maendeleo nchini

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameishukuru ya Serikali Jamhuri ya Watu wa China kwa kusaidia sekta ya afya ikiwemo vifaa tiba, miundombinu ya afya, dawa, mafunzo katika sekta ya afya kwa nyanja mbalimbali na timu ya madaktari wanaokuja kutoa huduma za tiba Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akishuhudia utiaji wa Saini ya Ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China,wakisaini Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (kulia) na kushoto ni Balozi Mdogo wa China anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe. Zhang Zhisheng, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo Mei 16,2023.(Picha na Ikulu).

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Mei 16, 2023, katika hafla ya utiaji wa saini wa ushirikiano wa miradi mitano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Zanzibar iliyofanyika  Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Kasha mgeni wake Rais wa Taasisi ya “Chinese –African People’s Friendship Association (CAPFA)” Dkt. Li Bin, baada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji wa saini ya Ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo
Rais Dkt. Mwinyi ameshuhudia utiaji saini wa mradi wa Ushirikiano wa hospitali baina ya China na Afrika, Utafiti na udhibiti wa magonjwa ya kitropiki-Kichocho, Uchunguzi wa saratani ya shingo ya Uzazi na kituo cha matibabu ya Mama na Mtoto pamoja na msaada wa vifaa tiba. 

Hospitali zitakazonufaika na ushirikiano huo ni ya Mnazi Mmoja, Kivunge ,Chake chake na Abdallah Mzee.
Rais wa Taasisi ya “Chinese –African People’s Friendship Association (CAPFA)” Dkt. Li Bin akizungumza katika hafla ya utiaji wa saini ya Ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China,iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo.(Picha na Ikulu).
Naye, Rais wa Chinese-African People’s Friendship Association (CAPFA),Dkt. Li Bin amesema urafiki uliopo wa kihistoria kati ya China na Zanzibar pamoja na ujio wa ugeni kutoka China ni kuendelea kuboresha fursa katika utalii, kutatua maradhi sugu kwa wakina Mama na fursa za miradi mbalimbali Zanzibar kwa kunufaisha pande zote za ushirikiano wa nchi hizi na kuboresha huduma sekta ya Afya.

Vilevile Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imesaidia Zanzibar vifaa tiba na dawa zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.2 za kitanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news