Rais Dkt.Mwinyi ateta na viongozi wa ACT Wazalendo

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na kuteta na viongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo.

Viongozi hao ni Mwenyekiti, Mhe. Juma Haji Duni, Makamu Mwenyekiti ambaye ni pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud na Mhe.Zitto Kabwe.

Pamoja na mambo mengine yanayohusu ustawi wa Zanzibar kisiasa na kijamii, kupitia mazungumzo hayo yaliyofanyika Mei 18, 2023 Ikulu jijini Zanzibar viongozi hao wameafikiana kwamba ipangwe tarehe ya kuzindua rasmi kamati maalum itakayoundwa na wajumbe kutoka vyama vya CCM na ACT-Wazalendo ambavyo ndivyo vilivyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Lengo likiwa ni kuanza kujadiliana na baadae kupanga mpango wa utekelezaji wa ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa kufuatia Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliojadili maeneo mahsusi yanayoihusu Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news