Rais Dkt.Mwinyi atoa wito kwa wawekezaji

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa wawekezaji wanaokusudia kuanzisha biashara zao Zanzibar washirikiane na jamii katika kusaidia masuala mbalimbali kama vile elimu, maji na afya.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kwamba, wawekezaji wanapaswa kuona umuhimu wa kusaidia jamii inayowazunguka pale wanapowekeza, na kuhakikisha kwamba wanachangia kwa hali na mali ili kuboresha uhusiano wao na jamii hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi, alipokuwa akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Wilaya ya Kusini Unguja mara baada ya kufungua Masjid El - Marhoum Abdel Moneim Shahein iliyongwa kwa ufadhili wa Dk.Sharif Abdel Shahein kutoka nchini Egypt, hafla iliyofanyika leo kijijini hapo leo Mei 26, 2023. (Picha na Ikulu).
Ameyasema hayo leo Mei 26, 2023 baada ya sala ya Ijumaa katika ufunguzi wa msikiti wa Masjid El-Marhoum Abdel Moeim Shahein uliopo Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja.

Katika hotuba yake Rais Dkt.Mwinyi amebainisha kuwa nia na madhumuni ya msikiti huo ni kutoa fursa ya kufanya ibada na kuwafundisha vijana katika madrasa iliyopo msikitini hapo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news