Rais Dkt.Mwinyi azidi kuwakaribisha wawekezaji nchini

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akiwa katika mwendelezo wa ziara yake nchini Qatar, amekutana na viongozi wa Kampuni ya Power International Holding.

Katika mazungumzo ya pamoja, viongozi hao wameonesha kupendezwa na mradi wa umeme wa Zanzibar, kuashiria fursa kubwa za uwekezaji katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya Zanzibar.

Katika hatua nyingine ya ziara yake, Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Abu Issa Holding, Bw.Ashraf Abu Issa,

Ni kampuni inayojihusisha na uwakala wa usafirishaji watalii. Katika mazungumzo yao, Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa kampuni hiyo kuangalia uwezekano wa kuongeza idadi ya watalii Zanzibar na pia kuwashawishi wawekezaji wengine kuja kuwekeza katika visiwa vidogo vidogo vilivyopo Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news