Rais Dkt.Mwinyi: Naomba nimpuuze

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Mheshimiwa Dkt.Hussein Mwinyi amesema, wanaoendeleza propaganda za upotoshaji kuhusu mambo mbalimbali nchini ikiwemo kisiasa wanapaswa kupuuzwa.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Mei 30, 2023 Ikulu jijini Zanzibar katika vikao vya kawaida vya kila mwezi na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu nchi.

"Kuhusu ili la kwamba CCM haijawahi kushinda, ndiyo yale niliyoyasema, upuuzi haujibiwi, upuuzwa ili siwezi kulijibu, nani asiyejua mfumo wa uchaguzi wa nchi yetu, maana wengine wanajibu toka kwenye kura za maoni ndani ya CCM ah! kampewa tu na Mwenyekiti...

"Jamani kuna mwaka ambao ulikuwa wazi katika uchaguzi kuliko mwaka huu wa uchaguzi, mwaka huu wa uchaguzi kura zilipigwa hadharani na zimehesabiwa hadharani, imewahi kutokea ile?.

"Sasa mtu akianza kuzungumza maneno hayo ya ovyo unamjibu au unampuuza? Mimi kwa ili naomba nimpuuze kwa sababu halipaswi kusikilizwa achilia mbali kujibiwa," amefafanua Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi katika mkutano huo na vyombo mbalimbali vya habari, ambapo alitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yaliyoulizwa katika mkutano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news