Rais Dkt.Samia afunga mafunzo ya TRAMPA,TAPSEA

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeanza kutekeleza mpango wa kukifanya Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora kiweze kutumika kuwanoa Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu kwenye ngazi ya Shahada.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Pongezi na Shukrani kutoka TAPSEA na TRAMPA iliyokabidhiwa kwake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa mkutano wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).(Picha na Ikulu).

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amesema hayo Mei 27, 2023 wakati wa kufunga mafunzo ya pamoja ya Chama cha Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) katika viwanja vya Fumba jijini Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt.Samia amesema lengo la kupandisha hadhi chuo hicho ni kuandaa watendaji wenye weledi na viwango vya juu kwa kutumia mitaala mipya.

Rais Samia pia amewasisitiza Watunza Kumbukumbu na Nyaraka na Makatibu Mahsusi kufanya kazi kwa nidhamu, uadilifu na kuzingatia misingi ya utunzaji siri, miongozo na kuheshimu mipaka ya kiutendaji.

Vile vile, Rais Samia amewahimiza kufanya kazi kwa weledi katika taaluma zao na kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amewaelekeza Mawaziri wenye dhamana ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuzungumza na waajiri katika sekta binafsi ili kuwaruhusu na kuwasaidia wanataaluma kushiriki mafunzo hayo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mkutano huo kuwaleta pamoja Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka kwa ajili ya kupata mafunzo maalum yenye kuwaongezea tija na ufanisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news