TanTrade,GIZ kuwawezesha wafanyabiashara wanaovuka mipaka

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) wamekubaliana kushirikiana katika uwezeshaji wa sekta ya biashara hususani kwenye eneo la wafanyabishara wanawake na vijana wanaovuka mipaka.
Aidha, eneo lingine taasisi hizo mbili zimeonesha nia ya kushirikiana ni eneo muhimu la taarifa za biashara na kurahisisha wafanyabiashara kuzipata kwa njia rahisi.

Hayo yamebainishwa Mei 8, 2023 na Bw. Fortunatus Mhambe, Kaimu Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) alipokuwa akizungumza katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi za TanTrade zilizopo Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Barabara ya Kilwa Dar es Salaam.
Amesema kuwa,uwezeshaji huo unalenga zaidi Miradi ya Maendeleo kwa Wafanyabiashara Wajasiriamali wadogo waliopo maeneo ya mipakani ili kuwarahisishia kufanya biashara kwa ufanisi na kukuza biashara zao na uchumi kwa ujumla.

Sambamba na kuwezesha kwenye ukusanyaji wa hatua za uingizaji na uuzaji wa mazao na bidhaa mbalimbali nje ya nchi kwenye Mfumo wa Trade Information Portal. 
Naye Meneja wa Mradi kutoka GIZ, Bi. Claudia Hofmann amesisitiza kuwa, nchi ya Ujerumani ipo tayari kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Tanzania kwa kuwawezesha wafanyabiashara wadogo waliopo mpakani hususani wanawake na vijana.
Hivyo, imekuja na mpango mkakati wa kuwasaidia Wafanyabiashara hao kwa kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zao kwa uhuru na ufanisi zaidi.

“Programu hii inalenga kukuza biashara ndani na nje ya Tanzania hivyo tumejipanga kutoa mafunzo na kuwapa wadau wetu nafasi za kuonesha bidhaa zao, kuwajengea uwezo wa kufanya biashara kwa uhuru na ufanisi zaidi na pia tunatoa nafasi kwa wadau kupata masoko mbalimbali ya ndani na nje ya nchi,”amebainisha Bi.Claudia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news