Wanafunzi wa kike waneemeka kupitia Mfuko wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius K.yerere

NA DIRAMAKINI

MFUKO wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius K.Nyerere ulioanza kutoa ufadhali katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2013/14 umeendelea kuongeza hamasa na ufaulu kwa wanafunzi wa kike katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa katika masomo ya Hisabati na Sayansi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano uliokutanisha wadau wa mfuko huo uliofanyika katika kumbi za mikutano za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila, alisema kuwa mpaka sasa mfuko huo umetoa udhamini kwa jumla ya wanafunzi wenye ufaulu wa juu 72, ambapo kati ya hao 50 ni wanawake na 22 ni wanaume.

“Mafanikio haya yanaendana na lengo la mfuko la kuongeza ufaulu wa wanafunzi hasa wa kike katika masomo ya Sayansi na Hisabati. Haya ni mafanikio makubwa ya mfuko katika kuleta usawa wa kijinsia katika maeneo hayo nchini,” alisema Dkt. Kayandabila.

Aliongeza kuwa mkutano huo unatoa fursa ya kujuana, kubadilishana uzoefu katika mambo mbalimbali na kupata ushauri toka uongozi wa mfuko na BoT. “Mkutano huo unatoa fursa kwa wadau wa mfuko kujadilianakwa pamoja jinsi ya kuongeza ushirikiano kati yao, mfuko na Benki kuu ya Tanzania kwa ujumla,” alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news