Waziri atuhumiwa kuhujumu umeme Afrika Kusini

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Afrika Kusini anayesimamia Kampuni ya Shirika la Umeme ya Eskom anadaiwa alidhoofisha usimamizi wa juu, na kuvuruga juhudi za kumaliza mzozo wa nishati nchini humo, hayo ikiwa ni kwa mujibu wa madai ya Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Eskom, Andre de Ruyter.

Pravin Gordhan ambaye ni Waziri wa Mashirika ya Umma imeelezwa ili kuondoa hali ya sintofahamu, angethibitisha habari iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji, na wafanyakazi wa ngazi ya chini wa Eskom, De Ruyter alisema katika kitabu chake kipya cha "Truth to Power: My Three Years Inside Eskom."

Afrika Kusini imekuwa ikikabiliwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara, hali ambayo inazorotesha ukuaji wa uchumi.

"Kila niliposikia akiangalia mara mbili taarifa zangu na wafanyakazi wa Eskom, iliacha ladha mbaya kinywani mwangu,"de Ruyter aliandika katika sehemu iliyochapishwa Jumapili. "Ikiwa huniamini, sawa, lakini niambie kisha unifukuze kazi."

De Ruyter alisema katika mahojiano ya televisheni mwezi Februari, mwaka huu kwamba Eskom ilikuwa ikipoteza takriban randi bilioni 1 (dola milioni 52) kwa mwezi kutokana na ufisadi na wizi, kwa msaada wa watu wanaohusishwa na chama tawala cha African National Congress.

Siku moja baadaye, Eskom ilitangaza kwamba De Ruyter angeiacha kampuni hiyo mara moja. Msemaji wa Gordhan alikataa kutoa maoni yake, akiongeza kuwa waziri huyo atafika bungeni wiki ijayo.

Bodi mpya iliyoteuliwa mnamo Septemba 30,mwaka jana inadaiwa, "ilionesha mfululizo wake wa kutatanisha mapema", pia kudhoofisha watendaji wakuu wa Eskom, De Ruyter aliandika. "Wajumbe wa bodi mara nyingi huwaita wafanyakazi katika ngazi ya usimamizi wa kati, ngazi kadhaa chini ya bodi, ili kujua jinsi mambo yalivyokuwa."

Msemaji wa Eskom na dawati lake la vyombo vya habari hawakujibu mara moja jumbe za kutaka maoni baada ya kuombwa kufanya hivyo. (Daily Investor)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news