Waziri Balozi Dkt.Chana ateta na viongozi mbalimbali

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Kimataifa siku ya Mei 11, 2023 jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao ni pamoja na Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini, Bw. Leo Nascher, Naibu Balozi wa Hispania hapa nchini, Bw Jose Garcia na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO, Bw. Michel Toto.

Mazungumzo yao yamelenga kuimarisha mashirikiano katika Sekta ya Michezo, Sanaa katika filamu pamoja na uhifadhi wa historia kupitia Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Dkt. Emmanuel Ishengoma, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Dkt. Kiagho Kilonzo, Mratibu wa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, Bw. Boniface Kadili pamoja na Mwakilishi kutoka Idara ya Michezo, Bw. Benson Chacha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news