Royal Tour ya Tanzania yajibu tena kutoka China

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amesema, kufuatia juhudi za Serikali kutangza utalii duniani, zinazoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya The Royal Tour ambayo imeitangza Tanzania kimataifa, makampuni makubwa 14 ya mawakala yanayoongoza kusafirisha watalii,
Sambamba na vyombo vikubwa sita vya habari kutoka China wameingia nchini leo Mei 12, 2023, majira ya saa moja asubuhi tayari kuanza ziara maalum ya takribani wiki mbili hapa nchini.

Ujumbe wa mawakala hao na waandishi wa habari 40 umetua nchini kupitia Zanzibar na baadaye unatarajiwa kuzuru sehemu mbalimbali za Tanzania.
Miongoni mwa maeneo hayo ni hifadhi za Tarangire, Manyara, Serengeti, Ngorongoro, eneo maarufu la kihistoria duniani la Oldivai Gorge, miji ya Dar es Salaam, Arusha na kufanya mikutano kadhaa na wadau wa utalii nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, John Mapepele imefafanua kuwa, lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea fursa na vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na kufanya mazungumzo ya kibiashara na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii.
Pia, kuandaa makala za utalii na Mei 18, mwaka huu ndiyo siku maalum ya ahadi baina ya mawakala hao na wadau wa utalii ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

"Kwa sasa Tanzania inaliangazia soko la watalii wa China kama soko la kimkakati kwa kuwa takribani watalii milioni 155 hutoka China kwenda kutembelea nchi mbalimbali duniani kila mwaka kwa takwimu za Baraza la Utalii na Usafirishaji Duniani (WTTC).
"Takwimu hizo zinaonesha kuwa, watalii wa China ndiyo watumiaji wazuri wa fedha wanapotembelea maeneo mbalimbali ya utalii duniani,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, uratibu wa ziara hiyo ya mafunzo umefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii ikishirikiana na wadau mbalimbali wa utalii, Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ubalozi wa Tanzania nchini China, Benki ya NMB na Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news