WAZIRI UMMY: DAWA ZA KIDONGE MYEYUKO CHA AMOXICILLIN, ZINKI NA ORS HAZIUZWI, NI BURE

NA MWANDISHI WAF

WAZIRI wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewaelekeza Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri wasimamie kwa ukamilifu utoaji wa dawa za kidonge myeyuko cha Amoxicillin,Zinki na ORS kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, zinanunuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau na kusisitiza kuwa dawa hizo haziuzwi zinatolewa bure kwa wananchi.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2023/2024 kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma. 

Amesema katika kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023, Wizara ilinunua na kusambaza dawa kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) ya kidonge myeyuko cha Amoxicillin vidonge milioni 30.1, na dozi 94,300 za Zinki na ORS kwa ajili ya matibabu ya kuharisha.

“Naomba kutumia fursa hii kusisitiza kwamba dawa za kidonge myeyuko cha Amoxicillin,Zinki na ORS kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, zinanunuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau na dawa hizi hazipaswi kuuzwa.Hivyo, nawaelekeza Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri wasimamie suala hili kwa ukamilifu,” amesisitiza Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema ununuzi wa dawa hizi uliwezesha kuimarika kwa upatikanaji wa dawa za watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika vituo vya kutolea huduma kwa asilimia 90 ikilinganishwa na asilimia 85.3 katika kipindi hicho mwaka 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news