Rais Dkt.Mwinyi: Serikali imeanza kuajiri wauguzi na imeongeza nafasi za ajira kwa madaktari

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeanza kuajiri wauguzi na imeongeza nafasi za ajira kwa madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya.

Ameyasema hayo leo Mei 12, 2023 katika Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali imefanya jitihada kubwa kwa kuongeza bajeti ya sekta ya afya, kujenga miundombinu ya afya ikiwemo ujenzi wa hospitali za wilaya na mkoa pamoja na vituo vya afya Unguja na Pemba. Wakati huo huo, 
 
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema,Serikali imeendelea na juhudi katika ununuzi wa vifaa vya tiba na uchunguzi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akipokea risala ya Wauguzi kutoka kwa Muuguzi Bi.Saida Kheir Hamad katika sherehe ya Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani leo katika Ukumbi wa Idrisa Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news