Yanga SC yatetea ubingwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara

NA DIRAMAKINI

HATIMAYE Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imetetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa pili mfululizo baada ya kuigonga Dodoma Jiji FC mabao 4-2.

Ni kupitia mtaanange wa nguvu na wenye mvuto ambao umepigwa Mei 13, 2023 katika Dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamazi ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Licha ya Yanga SC kutangulia kwa bao la mshambuliaji Kennedy Musonda dakika ya 39, lakini kipindi cha pili Dodoma Jiji FC walitoka nyuma na kuongoza mabao 2-1 hadi dakika ya 70.

Aidha, Collins Okpare aliisawazishia Dodoma Jiji dakika ya 59 na Seif Abdallah Karihe akafunga la pili dakika ya 67, kabla ya Mudathir Yahya kuisawazishia Yanga SC dakika ya 70.


Mabao mawili ya ushindi ya Yanga FC yalifungwa na Farid Mussa dakika ya 88 na Mudathir Yahya dakika ya 90 ya mtanange huo.

Kutokana na matokeo hayo,Yanga SC wanafikisha alama 74 ambazo zinawahakishia ubingwa, kwani hata wakipoteza mechi mbili zilizosalia na mtani Simba SC hata akishinda zote mbili bado wataendelea kuongoza.

Yanga SC wamebakiwa na michezo miwili dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons ambayo itachezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news