Kitayosce FC yatinga Ligi Kuu ya NBC 2023/2024

NA DIRAMAKINI

KITAYOSCE FC imepanda daraja hadi Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Sports ya Tanga.

Ni baada ya mtanage wa nguvu ambao umepigwa Mei 13, 2023 katika Dimba la Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Timu ya Kitayosce imefikisha alama 60 ikiwa ni moja zaidi ya Pamba FC ambayo pia ilishinda mabao 2-1 katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza

Aidha, Kitayosce imeungana na JKT Tanzania, mabingwa wa Championship waliomaliza kwa alama 63.

Wakati huo huo, Pamba FC itakwenda kumenyana na Mashujaa FC iliyomaliza na alama 49 nafasi ya nne na mshindi wa jumla atakwenda kumenyana na timu iliyoporomoka kutoka Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kuwania kupanda.

Pia,Green Warriors imeichapa Pan Africans mabao 3-2, Mashujaa FC imeichapa Mbuni FC mabao 2-1, Ken Gold imeichapa Biashara United mabao 3-2 na Mbeya Kwanza imeichapa Copco FC mabao 4-3.

Nao Gwambina na Ndanda FC zilizojitoa ndio zimeshuka, wakati Copco, Green Warriors, Pan African na Africans Sports zitakwenda kwenye mchujo wa kuwania kubaki Championship.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news