VIDEO:Chongolo awamegea siri wana Kondoa

NA DIRAMAKINI

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo amewataka wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma kuendelea kuwapeleka watoto wao shule, kwani vijana wengi wilayani humo Mungu amewakirimia vipawa vya kipekee.

"Mimi nitoe wito kwenu, kwenye elimu pelekeni vijana wakasome. Ninyi hapa Kondoa moja ya sifa kubwa ya hapa Kondoa vijana mkiwapeleka shule ni wazuri wa namba, hesabu, wanajua hesabu kweli kweli ni wazuri kweli kweli kwenye uchumi. 

"Na vijana wengi kuanzia mwenyekiti wenu wa mkoa, vijana wilaya yenu vichwa inachemka. mkiwapeleka mtakua na tija kubwa kwa nchi hii.
"Wengi ambao wameenda ninyi wenyewe ni mashaidi, hapa tumepata watu wazito, kwenye majeshi ya ulinzi, kwenye polisi, kwenye magereza, kwenye fedha kwenye kila eneo la nchi hii kuna watu waliotoka Kondoa. Kwa sifa yenu kubwa ni uaminifu. Watu wa Kondoa ni waaminifu, lakini tumewazidi kidogo wa Iringa."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news