Dkt.Mwinyi:Hakuna uhai katika chama kama hakuna umoja

NA DIRAMAKINI

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Jumapili tarehe 4 Juni, 2023 ameendelea na ziara ya kichama katika Mkoa wa Kusini Unguja na kuzungumza na viongozi wa Mashina, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ngazi ya Majimbo, Wilaya na Mkoa.
Katika hotuba yake, Rais Dkt. Mwinyi amesema, "hakuna uhai katika chama kama hakuna umoja tunachotakiwa kufanya hivi sasa ni kuondoa tofauti zetu ili kuimarisha umoja wetu." 
Aidha, amesema daftari la wapiga kura ni muhimu katika uhai wa chama. "Viongozi wa ngazi zote tuhakikishe tunahakiki daftari la wapiga kura kujua idadi ya wanachama." 
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Juni 4, 2023 katika muendelezo wa ziara zake za kutembelea mikoa mbalimbali tangu achaguliwe kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news