Hongera Young Africans Sports Club kwa heshima mliyolipa Taifa letu

NA MWALIMU MEIJO LAIZER

NI dhahiri kuwa, Young Africans Sports Club imetupa heshima kama nchi kwa kupigana kufa na kupona katika Ardhi ya Waarabu na kupata ushindi ugenini japo kwa sheria gandamizi za CAF imetutoa katika nafasi ya kuchukua Kombe la Shirikisho la CAF.

Katika kuperuzi mitandao ya kijamii nimekuta na kauli mbalimbali za Watanzania wazalendo, mmoja akisema hivi, "Jana ndio nimejua kwa nini FIFA na Ulaya (UEFA) wamefuta hiyo sheria ya goli la ugenini kukupa ushindi. Sijawahi ona timu iliyotoka uwanjani ikiwa na ushindi tena ushindi ulioiwezesha kupata aggregate sawa na mwenzake inanyimwa kombe kwa sheria za kipuuzi!!!,

"FIFA na UEFA wamefuta sheria ya goli la ugenini,na CAF wafute!!! Yote kwa yote ningekuwa dar ningefika uwanja wa ndege mapema kuipokea Yanga!!!Imeleta heshima ya nchi!!!."

Nami naweza kusema vita ya Young Africans Sports Club na USM Alger jana imeonesha uwezo mkubwa wa TIMU YA WANANCHI yaaani Yanga kwa kuipiga Timu ya Waarabu nyumbani kwao bila huruma.

Hii imetupa heshima kubwa kama Taifa japo wapo wenzetu wasio na uzalendo wanaobeza ushindi wa jana uliopatikana katika Ardhi ya Ugenini.

Awali nimesema kuwa Vita ya USM Alger na Young Africans ni Vita ya Tanzania na Algeria katika soka, wengine walibisha nakuonesha kuwa hii siyo vita ya nchi yetu na Algeria bali ni vita ya USM Alger na Young Africans tu.

Kwenye mitandao ya kijamii watani wetu wa jana, wengi wao wanabeza ushindi wa Yanga Africans katika Ardhi ya Waarabu bila kuangalia tofauti ya Fainali za Kombe la Shirikisho la CAF 1993 na Fainali hizi za Kombe la Shirikisho la CAF 2023.

Young Africans imeandika rekodi mpya kwa Serikali ya Awamu ya Sita jambo ambalo sote tuna kila sababu ya kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha mtazamo chanya katika Sekta ya Mchezo na kufanya Young Africans kufika Hatua ya Fainali za Kombe la Shirikisho la CAF.

Sambamba na kuonesha kiwango kikubwa katika ubora wake kwa Bara la Afrika sote katika hili tunaipongeza Timu ya Young Africans kwa hatua waliofikia.

Young Africans kupata mchezaji Bora na Man of the Match hii ilikua vita kubwa na awali nimesema kuwa hii vita ya USM Alger na Young Africans katika soka na watani wetu wameona.

Uongozi wa Young Africans, Professor Nabi na benchi lake la ufundi amekua mwalimu mzuri kwa kila hatua na kufanya Young Africans kuwa timu ya pekee katika nchi yetu na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuandikwa katika Vitabu vya Historia vya FIFA na CAF ili kusaidia kumbukumbu kwa vizazi na vizazi vijavyo.

Young Africans mtabaki kuwa Mashujaa wa Taifa Letu kwa hatua mliyofikia na kufanya Taifa letu kuwa moja za nchi zenye viwango bora katika Sekta ya Mchezo ya Mpira ya Miguu.

Katika safari yenu ya kurejea nchini natumia fursa hii kuwakaribisha kwa upendo na furaha kubwa kama mashujaa wa Taifa Letu, kama wapiganaji hodari kwa Taifa Letu, kama wazalendo muhimu kwa Taifa Letu.nchi inatambua kazi kubwa mliyofanya katika ardhi ya Waarabu, kongole kwenu wote.

Mwalimu Meijo Laizer
Mshabiki wa Yanga
kutoka jijini Arusha

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news