JKCI yatangaza upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo Pemba

NA MWANDISHI WETU

WATAALAMU wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee iliyopo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba watafanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Kisiwa cha Pemba.

Mtaalamu wa kupima vipimo vya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Paschal Kondi akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mkazi wa Manyara wakati wa kambi maalum ya upimaji wa moyo iliyofanyika Machi, mwaka huu mkoani humo.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano JKCI, Anna Nkinda leo Juni 6, 2023.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, upimaji huo utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia Juni 19,2023 hadi Juni 23,2023 saa mbili kamili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo,kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

"Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

"Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

"Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa namba 0777905996 Dkt. Mohamed Faki Saleh na 0777509060 Dkt. Rashid Saleh Hemed.Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news