Kamishna Jenerali Aretas Lyimo aguswa na huduma inayotolewa kwa waraibu Hospitali ya Mount Meru

NA MWANDISHI WETU

KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo leo Juni 27, 2023 ametembelea Kliniki ya Tiba Saidizi kwa waraibu (Methadone) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru na kuangalia huduma inayoendelea kutolewa kwenye kliniki hiyo.
Aidha, ameupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuendelea kutoa huduma za tiba kwa Waraibu na kueleza kuwa mamlaka itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwenye kliniki hiyo.

Naye Mganga Mfawidhi wa Mount Meru, Dkt. Alex Ernest ameishukuru mamlaka kwa kuendelea kutoa misaada kwenye kliniki hiyo kuanzia ujenzi wa jengo la kliniki, samani pamoja na vifaa tiba vinavyorahisisha uendeshaji wa huduma hiyo.
Ameongeza kuwa, hosptali hiyo imefanikiwa kutenga eneo la mafunzo ya kilimo cha mbogamboga ili kuwasaidia waraibu kupata ujuzi na kutumia kama fursa ya kujipatia kipato.

Akisoma risala fupi mbele Kamishna Jenerali Mkuu wa Kitengo cha Methadone Dkt. Salum Said ameeleza kuwa,kliniki ya tiba saidizi ya waraibu (Methadone) ni kliniki inayotoa dawa ya Methadone kwa waraibu wa dawa za kulevya kwa mikoa mitatu Arusha, Kilimanjaro na Manyara na kwa kipindi cha miaka miwili tangu ianzishwe imehudumia waraibu wapatao 616, wanaume wakiwa ni asilimia 82 na wanawake asilimia 18.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news