'Lowassa' aunga mkono maono ya Rais Dkt.Samia

NA DIRAMAKINI

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Sabiniani maarufu Lowassa amekuja na daraja jipya ambalo ni kiunganishi kati ya vijana na wadau mbalimbali nchini ili kuweza kuziendea fursa za ajira kwa kujiajiri wenyewe.
Mwasisi wa maono hayo,Charles Sabiniani maarufu Lowassa (wa tano kutoka kulia aliyevalia skafu ya bendera ya Taifa) akiwa na wadau mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam wakiwa wameshikilia nembo ya jumuiya.

Ikiwa ni jitihada za kuunga mkono maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuwaunganisha Watanzania na fursa mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi. 

Ni kupitia Jumuiya ya Mama Enterprises ambayo, Sabiniani maarufu Lowassa ameianzishwa mwaka jana mwishoni, lakini utekelezaji wa maono yake ya kuzifikia fursa ikiwa imeshirikisha Watanzania mbalimbali umeanza sasa. 

"Nikiwa kijana mpenda maendeleo ya taifa letu mwaka jana niliamua kuwatembelea watumishi mbalimbali wastaafu wakiwemo viongozi wa Serikali na sekta binafsi,watumishi walioko kwenye majukumu sasa, wachungaji, mashehe na wanavyuo kama Chuo cha Diplomasia.

"Wafanyakazi taasisi za elimu ya fedha, afya, wafanyabiashara wadogo na wakubwa na wajasiriamali mbalimbali nilifanya hivi ili kupata Watanzania baadhi wanaounga mkono juhudi za Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake nchi nzima 

"Niliwapa maono yangu ili kuwa mwongozo wa kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa vitendo moja ya maono ni kujiandaa kuingia mashambani kulima,"amefafanua Sabiani maarufu Lowassa leo Juni 24, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wakizindua nembo ya jumuiya hiyo na kauli mbiu yao ya 'Tuko tayari kuleta maendeleo endelevu'.

Uzinduzi huo ambao mgeni rasmi alikuwa Mhandisi Kiboko Manyerere Nyerere kutoka kwenye familia ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pia wadau mbalimbali walishiriki.

Miongoni mwao ni Subrina Said Gwando ambaye ni Katibu Mkuu wa Jukwaa la Watoto Tanzania,Dkt.Magrose Kavura Majige kutoka Jukwaa la Akili na Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wengine, mbali na maafisa mbalimbali wa Serikali wastaafu na watumishi wengine pia walikuwepo maafisa kutoka Benki ya Azania, Theodosia na Magege ambao wameonesha nia ya kuunga mkono Jumuiya ya Mama Enterprises na kuhakikisha wanaleta maendeleo endelevu wakiunga mkono juhudi za Serikali chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Pia, alikuwepo Mchungaji Dorah S. Temba ambaye ni Mjumbe Kamati ya Utendaji ambapo kwa pamoja wameonesha kuguswa na maono hayo chanya kwa ustawi bora wa jamii na Taifa kwa ujumla.

Sabiniani maarufu Lowassa amesema,kupitia jukwaa hilo wanatarajia kuanzia sasa hadi 2026 wawe tayari wametengeneza ajira zaidi ya 10,000,

"Kwa hiyo, tukishalima tutaleta kwenye jumuiya yetu ili wanajumuiya wapate unga, mchele na kuendelea kwa bei nafuu hapo tutakuwa tumeongeza ajira na kupunguza ukali wa maisha kupitia sisi wanajumuiya.

"Na baadhi yetu wawe wasambazaji wa bidhaa zetu kwenye jamii hapo tutakuwa tumetengeneza ajira pia jumuiya isababishe mwana jumuiya kumiliki mradi wake mwenyewe nikitegemea kufika 2026 jumuiya yetu itengeneze ajira 10,000 kwa Watanzania, nikiamini tutakuwa tumeipunguzia mzigo Serikali wa watu wasio na ajira,"amefafanua Sabiniani maarufu Lowassa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news