Naibu Spika Mheshimiwa Zungu mgeni rasmi Maonesho ya Wizara ya Utamaduni

NA ELEUTERI MANGI-WUSM

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu anatarajiwa kufungua maonesho ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na taasisi zake yatakayofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Juni 5 hadi 6, 2023 katika viwanja vya Bungeni jijini Dodoma. 
Akikagua maandalizi mabanda yatakayotumika kwenye maonesho hayo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu amesema wizara hiyo ambayo ni nguvu shawishi ya Serikali itatoa fursa kwa Wabunge kujifunza na kuona kwa vitendo kazi zinazofanywa na Wizara hiyo kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti yake Juni 6, 2023.
Bw. Saidi Yakubu anawakaribisha Waheshimiwa Wabunge na wageni wote wa Bunge kutembelea mabanda ya Wizara hiyo pamoja na taasisi zake ili kupata huduma zinazotolewa na wizarani hapo na taasisi zake.
Aidha, Wizara hiyo itatumia fursa hiyo kutoa baadhi ya vifaa vya michezo kwa waheshimiwa Wabunge pamoja na vitendea kazi vingine ambayo vinatumika kurahisisha utendaji kazi wao wa kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news