Prof.Muhongo atoa mapendekezo ya kukoleza kasi ukuaji uchumi

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Mkoani Mara Prof.Sospeter Muhongo amesema, kupatikana kwa umeme wa uhakika nchini kutachochea kwa kasi ukuaji wa uchumi katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo. 
Prof. Muhongo ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma leo Juni 19, 2023 wakati akitoa mchango wake kuhusu hali ya uchumi na mpango wa maendeleo ikiwemo bajeti ya 2023/2024.

Amesema,umuhimu wa uchumi kukua kwa zaidi ya asilimia 8 kwa mwaka (8-10% growth) umeme mwingi, wa uhakika na wa bei nafuu unahitajika.

Prof. Muhongo amebainisha kwamba,umeme kwa sasa bado haujatosha ambapo megawati 10,000. zinahitajika ili kufikia kiwango cha uhitaji.Tazama video hapa chini;
Amesema, Tanzania inahitaji umeme mwingi wa uhakika ikiwa ni pamoja na vyanzo vingi vya upatikanaji wake.

Katika mchango wake huo, pia Prof.Muhongo amependekeza kupunguzwa kwa bei ya umeme ili kuweza kuwapata watumiaji wengi zaidi.

Amesema, kitu kingine kitakachopelekea uchumi kukua kwa kasi ni pamoja na uchumi wa gesi ukitumiwa vizuri.

"Kingine kitakachofanya uchumi ukue kwa kasi na umasikini kutokomea ni lazima tuwekeze kwenye gesi na mafuta na hapo ndio tutaweza kufikia malengo,"amesema Prof.Muhongo.

Amesema, anaiunga mkono hoja kwa kuwa Musoma Vijijini ipo miradi ambayo inakwenda kuanza mwezi wa 8 ikiwemo ya barabara na kilimo cha umwagiliaji ambayo itakwenda kuinua uchumi wa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news