Dkt.Msonde asisitiza uadilifu kwa watumishi OR-TAMISEMI

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI

KAIMU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Charles Msonde amewataka watumishi wa ofisi yake kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kutekeleza azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa na utumishi wa umma wenye uadilifu na tija katika maendeleo ya taifa. 
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akizungumza na watumishi wa ofisi yake mara baada ya kumpokea Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila.

Dkt. Msonde ametoa wito huo leo kwa watumishi wa TAMISEMI mara baada ya kumpokea Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila alieapishwa tarehe 16, Juni 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma. 
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akimkabidhi vitendea kazi Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila mara baada ya kuripoti Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Dkt. Msonda amesema, watumishi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwani wanatekeleza majukumu yao kwa niaba ya mwenye dhamana ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

“Dhamana tuliyopewa ya kuitumikia ofisi hii inatulazimu kuwa mstali wa mbele katika kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kiutumishi iliyopo, hivyo tunapaswa kuhakikisha tunafanya kazi kwa uadilifu ili tusimuangushe Mheshimiwa Rais,”Dkt. Msonde amesisitiza. 
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akiongoza kikao kazi cha Menejimenti kilichoandaliwa kwa lengo la kumtambulisha Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila aliyeripoti ofisini leo.

Naye, Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Mahera amemshukuru Mhe. Rais kwa kumteua Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila ili kuongeza nguvu ya kiutendaji katika Ofisi ya Rais-TAMISEMI na kuongeza kuwa, ni wajibu wa menejimenti kuhakikisha inafanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo. 
Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila akipokea zawadi ya ua toka kwa mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi. Angela Mgemela mara baada ya Naibu Katibu Mkuu huyo kuripoti ofisini. Wanaohududia ni viongozi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila ameiomba Menejimenti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kumpa ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu. 
Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuripoti Ofisi ya Rais-TAMISEMI. Anayeshuhudia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Menejimenti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. John Cheyo amesema Menejimenti itatoa ushiriano wa dhati kwa Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila ili aweze kutimiza wajibu wake ipasavyo. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news