Rais Dkt.Mwinyi awasili jijini Berlin

BERLIN-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Brandenburg jijini Berlin, Ujerumani na kupokewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi.

Rais Dkt.Mwinyi ameambatana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Mwita, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Dkt.Mwinyi atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu (Special Olympics World Games) ambayo maelfu ya wanamichezo wenye mahitaji maalumu kushindana katika michezo mbalimbali, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Juni 17 hadi 25 Juni 2023.

Mbali na kushiriki uzinduzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu jijini Berlin, Rais Dk, Mwinyi pia atakutana na viongozi wa juu wa Serikali nchini humo, Wakuu wa Mashirika mbalimbali, Wawekezaji na jamii ya Watanzania waishio Ujerumani (Diaspora).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news