Rais Dkt.Samia afanya uteuzi, mabadiliko ya vituo vya kazi

NA GODFREY NKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amewateua viongozi na kufanya mabadiliko madogo ya vituo vya kazi.

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa leo Juni 9, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw. Tito Philemon Mganwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.

Pia,amemteua Bw. Mussa R. Kilakala kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora huku akifanya mabadiliko madogo ya vituo vya kazi.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemuhamisha Athumani Francis Msabila kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.

Bi.Mwantum Hamis Mgonja kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Bi. Mwamvua Bakari Mnyongo kutoka Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora kwenda kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news