Rais Dkt.Samia ateua watatu kuwa na Hadhi ya Balozi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao kuwa na Hadhi ya Balozi kama
ifuatavyo:-
1. Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Balozi;
2. Dkt. Salim Othman Hamad, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya Siasa kuwa Balozi; na
3. Dkt. Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya Hotuba kuwa Balozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 13, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus,uteuzi huu wa Hadhi ya Balozi umeanza Juni 12, 2023.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo vyeo walivyonavyo vinabaki kama vilivyo na wateule wataapishwa Juni 16, 2023 kuanzia saa 04:00 asubuhi Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news