Serikali yaahidi mema zaidi kwa wawekezaji nchini

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwaenzi, kuwalinda na kuwatunza wawekezaji wanowekeza nchini. 
Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa pamoja na uongozi wa Mkoa wa Iringa na wakitembelea Kiwanda cha Yisen International Company kilichopo Mufindi Iringa Juni 24, 2023 baada ya kusikiliza changamoto za Wamiliki wa Viwanda hivyo. Kiwanda hicho kinachozalisha Plywood, Marine Boards na MDF kwa kutumia malighafi ya vinia inayotokana na miti.

Aidha, ametoa rai kwa Wawekezaji kuendelea kuwekeza kwa kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI).

Dkt. Abdallah ameyasema hayo kwa Juni 24,2023 mkoani Iringa Wilaya ya Mufindi alipokutana na kusikiliza changamoto za Wamiliki wa Viwanda vya kuzalisha bidhaa za mazao ya misitu hususani Vinia inayotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama plywood MDF, na marine boards.
Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa pamoja na uongozi wa Mkoa wa Iringa na akiangalia marine board zinazotengenezwa na malighafi za vinia alipotembelea Kiwanda cha East Africa Shenyuan Group kilichopo Mufindi Iringa Juni 24, 2023 baada ya kusikiliza changamoto za Wamiliki wa Viwanda hivyo. Kiwanda hicho kinachozalisha Plywood, Marine Boards na MDF kwa kutumia malighafi ya vinia inayotokana na miti.

Akisikiliza changamoto zao baada ya kutembelea baadhi ya Viwanda vikubwa vinavyozalisha Vinia mpaka zao la mwisho na vidogo vinavyozalisha vinia peke yake, Dkt. Abdallah amesema Wizara kwa itashirikiana na Mkoa wa Iringa pamoja na Wakala wa Misitu (TFS ) kutatua changamoto zote zilizojitokeza ili wawekezaji hao waendelee kuzalisha bidhaa hizo kwa tija.
Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa pamoja na uongozi wa Mkoa wa Iringa na wakiangalia kipande cha vinia aliptembelea Kiwanda cha Cheda Mas Wood kilichopo Mufindi Iringa Juni 24, 2023 baada ya kusikiliza changamoto za Wamiliki wa Viwanda hivyo. Kiwanda hicho kinachozalisha malighafi ya vinia inayotokana na Miti na kuviuzia viwanda vingine kutengeneza bidhaa za mwisho.

Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Bi. Asifiwe Mwakibete ametoa kwa wawekezaji kuendelea kuwekeza katika viwanda vya mazao ya misitu mkoani humo kwa kuwa malighafi ya miti inapatikana kwa wingi na wananchi waendelee kupanda miti kwa kuwa soko la miti ya mbao ni kubwa mkoani humo.
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Yisen International Company kilichopo Mufindi Iringa wakiendelea na kazi ya uchakataji wa vinia inayotumika kutengeneza plywood, marine boards, samani, vifaa vya michezo, makasha ya kusafirisha bidhaa na ujenzi wa majengo na miundombinu mbalimbali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Bw.Ayoub Kambi amesema kwa kushirikiana na Mkoa wa Iringa wataweka mikakati ya kutatua changamoto zote zilizojitokeza kwa wawekezaji wa viwanda vinavyotengeneza bidhaa kwa kutumia Vinia

Vinia ni moja ya mazao ya misitu yanayohandisiwa ( Engeneered Wood Products(EWP) inayotumika kutengeneza moja kwa moja bidhaa za mazao ya mbao. Vilevile hutumika kutengeneza plywood, marine boards, samani, vifaa vya michezo, makasha ya kusafirisha bidhaa na ujenzi wa majengo na miundombinu mbalimbali.
Wamiliki wa Viwanda vinavyotengeneza Vinia na na bidhaa zinazotokana na malighafi hiyo wakitoa changamoto zao mbalimbali mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Uongozi wa Mkoa wa Iringa uliojumuisha Mji wa Mafinga, Wilaya ya MufindiI, TIC, TFS na TRA, Juni 24, 2023.

Wilaya ya Mufindi ina viwanda 27 vinavyoshughulika na uzalishaji wa vinia. Kati ya hivyo viwanda 6 vinauwezo wa kuzalisha bidhaa hadi hatua ya mwisho kama plywood MDF na marine board kwa kutumia vinia na viwanda vingine vinaishia hatua ya malighafi ya vinia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news