Mbinga Coffee Curing Company Co Ltd (MCCCO) yawapa tabasamu wakulima wa kahawa

NA MWANDISHI WETU

KIWANDA cha Chama Kikuu cha Wakulima wa zao la Kahawa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma (Mbinga Coffee Curing Company Co Ltd (MCCCO) kwa msimu wa mwaka 2022/2023 kimefanikwa kupokea kahawa na kukoboa kutoka kwa wakulima zaidi ya tani 18875.
Picha ikionesha mashamba ya kahawa ya wakulima katika Kijiji cha Langilo Kata ya Langilo bonde la Hagati Maguu Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Kati ya tani 18,000 ya uzalishaji wote ambapo tani zilizosalia zilichukuliwa na viwanda vingine vinavyojihusisha na ukoboaji.

Meneja mkuu wa kiwanda hicho, Festo Chang'a amesema kuwa, kiwanda hicho kinakutana na changamoto nyingi za upokeaji kahawa kutoka kwa wakulima kutokana na vyama vingi vya msingi AMCO’S kutotambua kwamba kiwanda hicho ni mali yao na hivyo wanapaswa kupeleka kahawa kwa wingi katika kiwanda hicho badala ya kupeleka viwanda vingine.

Chang'a amesema kuwa, kwa vile kwa sasa kiwanda hicho kinakabiliwa na ushindani mkubwa amewataka AMCO’S hizo kupeleka kahawa katika kiwanda chao ambacho wanahisa nacho ili kujiongezea kipato kwenye ushirika wao.

Sambamba kupata fursa mbalimbali ambazo zinatolewa kiwandani hapo kama vile kuongeza nguvu wakati wa kuhudumia mashamba ya kahawa hiyo ikiwa mashambani ili kupata kahawa iliyo bora.

Amesema kuwa, kiwanda hicho pia husaidia shughuli za maendeleo katika vijiji ambavyo AMCO’S zao zimepeleka kahawa katika kiwanda hicho kama vile kuchangia saruji,mabati kwenye ujenzi wa shule za sekondari, shule za msingi na zahanati pamoja na majengo ya ofisi za vijiji au kata kwa pale inapobidi.

Aidha, amesema kuwa kiwanda hicho pia hutoa ajira kubwa kwa wakazi wa Mbinga na wilaya jirani ambapo vijana wengi wa kiume na wa kike hupata ajira hiyo ya msimu na kujipatia kipata badala ya kuzurura.

Pia, amesema kama kahawa hiyo haipelekwi kwa wingi kiwandani hapo husababisha kuwepo kwa upungufu mkubwa wa ajira hasa kwa akinamama na akinababa.

Hata hivyo, amesema kuwa kwa msimu wa mwaka 2023/2024 kiwanda kimejipanga kikamilifu kuhakikisha kinapata kahawa kwa wingi kutoka katika AMCO’S na vikundi mbalimbali vinavyojishughulisha na uzalishaji wa zao la kahawa na kukoboa kwa wakati kwa kadri ya mahitaji yao.

Ka upande wake afisa masoko wa kiwanda hicho, David Haule amesema kuwa, kiwanda hicho pia kinajishughulisha na usindikaji wa kahawa inayozalishwa Mbinga ambayo inakuwa na ubora mkubwa na safi kwa matumizi ya kunywa na hivyo kukifanya kiwanda hicho kuendelea kuwa na ubora zaidi kutokana na kuhamasisha wakulima pamoja na wananchi kwa ujumla kunywa kahawa inayolimwa na wenyewe.

Haule amesema kwamba, baada ya kusindika kahawa hiyo nyingine husambazwa katika maeneo mbalimbali hapa Tanzania kama vile mikoa ya Dodoma, Dar es salaam, Tanga, Lindi, Mtwara, Iringa na Mbeya ikwa ni pamoja na maeneo mengine ambayo hayajatajwa na kwamba kahawa hiyo inapatikana kiwandani hapo kwa wale watakaohitaji kunywa kahawa yenye ladha nzuri na ndiyo inayopendwa duniani kote inapatikana muda wote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news