Serikali yadhamiria makubwa soko la zabibu

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Sulu Hassan imeainisha mikakati katika kuhakikisha soko la zabibu linakuwa la uhakika ndani na nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde amesema hayo leo Juni 18, 2023 katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Daniel Chongolo ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika Mkoa wa Dodoma ambapo ametembelea Mradi mkubwa wa Umwagiliaji wa Chinangali.

Mavunde amesema mikakati ya Wizara hiyo ni kuhakikisha wanatafuta masoko ya zao la zabibu ikiwa ni pamoja na kuanzisha kiwanda cha kuchakata zao hilo ili kuwa na uhakika kuhifadhi mchuzi wa zabibu kwa muda mrefu.
Mkakati mwingine ni pamoja na kutoza kodi kwa mvinyo kutoka nje ya nchi ili kuimarisha soko la ndani na kuendelea kuhamasisha wawekezaji katika wa ujenzi matanki makubwa ya kuhifafhi mchuzi wa zabibu.

"Serikali imepata mwekezaji mkubwa atakae kuwa anatengeneza juisi na atanunua zabibu kwa wingi. Pia tuko kwenye mazungumzo na TBL waweze kuhifadhi mchuzi wa zabibu kwa muda mrefu," Mavunde amefafanua.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo ameiagiza Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango kukutana na kuona fedha zinapatikana na wakandarasi wanalipwa kwa wakati ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji.
"Dhamira ya Rais Samia na Serikali yake kwenye hii miradi ya uwagiliaji ni kuona tija inapatikana kwa haraka, sasa nendeni mkakae na mje na majibu ndani ya muda mfupi kuhusu mbinu ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hii ambayo ina dhamira ya kujenga uhakika wa Kilimo kwa wananchi ili malengo ya Rais na Serikali anayoiongoza yafikiwe kwa muda uliokusudiwa na si vinginevyo.

"Hatutakuwa na maana kama tutakuwa na miradi yenye majina mazuri yenye dhamira njema na isilete matokeo kwa wakati,"amefafanua Chongolo.
Aidha, Changolo pia amekitaka Chama cha ushirika wa Kilimo cha zabibu, kuanzisha Mfuko ambao utatumika kufanya matengenezo kwenye miundombinu ya umwangiliaji katika mashamba ya ushirika huo.

Kuhusu soko la zabibu, Chongolo amewataka kutofikiria ununuzi wa zabibu kutoka nje bali kuwa na uzalishaji wa bidhaa ya mwisho wa zao la zabibu ndani ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news