Taifa Stars yaibamiza Niger 1-0, yafufua matumaini AFCON 2023

NA ELEUTERI MANGI

TIMU ya soka ya Tanzania, Taifa Stars imeicharaza timu ya Niger goli 1-0 na kufufua matumaini ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023 nchini Ivory Coast.
Saimon Msuva mfungaji wa goli hilo ndiye shujaa wa mchezo huo uliochezwa Juni 18, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amewaongoza watanzania kuishangilia timu yao akiwa Mgeni Rasmi katika mchezo huo hatua iliyoongeza hamasa.
Mchezo huo umeshuhudiwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu na Naibu Katibu Mkuu wake Bw. Nicholas Mkapa, Rais wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF), Wales Karia.
Tanzania ipo kundi F pamoja na timu za mataifa ya Algeria, Niger na Uganda kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news