Serikali yataja sababu ya kuwanoa mawakili wake nchini

NA MWANDISHI MAALUM

SERIKALI imesema imewanoa wawakili wake ili wakapunguze mrundikano wa kesi mahakamani. Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi.Mary Makondo wakati akifunga mafunzo kwa wakili wa Serikali yaliyotolewa kwa siku tatu kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akisalimiana na Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniphace Luhende mara baada ya kufunga mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kutoka Wizara, Taasisi, Idara, Mikoa na Halmashauri zote nchini. Mafunzo hayo yameandaliwa na OWMS.(Picha na OWMS).

Bi.Makondo amewaeleza mawakili hao wa Serikali kuwa, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeratibu na kufadhili mafunzo kwa mawakili hao wa wizara, taasisi, idara na halmashauri zote nchini kote ambapo yaligusa maeneo mbalimbali ikiwemo utatuzi wa migogoro.

Mbali na migogoro ni masuala ya ufilisi, uamuzi na usuluhishi, usuluhishi wa Kimataifa na Kitaifa, mbinu za kuzuia migogoro, mikataba ya uwekezaji, afya ya akili, matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na akili bandia katika uendeshaji wa mashauri.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya OWMS pamoja na Mawakili wa Serikali kutoka wizara, taasisi, idara, mikoa na halmashauri nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi Mary Makondo (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo kwa mawakili hao yaliyofanyika jijini Dodoma.

"Serikali imewanoa mka[unguze mrundikano wa kesi mahakamani katika kutatua migogoro pale ambapo migogoro hiyo haiepukiki ya kibiashara, wawekezaji, uwezo wa kuzuia au kukwepa migogoro, kufanya majadiliano ili kuitetea na kuiwakilisha Serikali mahakamani na kwenye mabaraza mbalimbali kwa kuwa Serikali imewaamini, hivyo mkajenge imani kwa wawekezaji,"amesema Bi.Makondo.

Pia, amewataka mawakili wote wa Serikali kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na mgeni rasmi, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akifungua maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na mafunzo kwa mawakili wa Serikali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Marry Makondo akizungumza na Mawakili wa Serikali (hawapo pichani) wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa mawakili wa Serikali yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Vile vile, Katibu Mkuu ameipongeza Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa kufanya maadhimisho ili kuweza kufanya tathimini ya utekelezaji wa majukumu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi kwa manufaa ya umma kwa kuwa, Serikali inategemea Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika kutetea Serikali.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende akizungumza na Mawakili wa Serikali (hawapo pichani) wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo (hayupo pichani) ili aweze kufunga mafunzo kwa mawakili hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma.

Akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Bi.Makondo kufunga mafunzo hayo, Wakili Muu wa Serikali, Dkt.Bonipgace Luhende amesema,ofisi inashukuru kwa ushirikiano iliyopata kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na kutoka kwa wizara, idara, taasisi za Serikali na halmashauri zote nchini kwa kuridhia kuwawezesha na kuwaruhusu mawakili wa Serikali kushiriki mafunzo hayo.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Sarah Mwaipopo akizungumza na Mawakili wa Serikali wakati wa kufunga mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kutoka Wizara, Taasisi, Idara, Mikoa na Halmashauri zote nchini yaliyofanyika jijini Dodoma.

Naye Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi.Sarah Mwaipopo amewashukuru wafadhili na wadau mbalimbali waliowezesha mafunzo hayo kufanyika kwa siku tatu mfululizo na zaidi ya mawakili 600 wamepata mafunzo hayo kwa ufanisi mkubwa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza kwa niaba ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bi.Faruma Idd ameishukuru Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa kuialika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushiriki katika mafunzo hayo.

Amesema, wataendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali na imani yake ni kwamba, mafunzo hayo yatawasaidia mawakili wa Serikali katika utendaji kazi.

Pia, amewapongeza na kuwashukuru watoa mada na wakufunzi wote walioendesha mafunzo hayo huku akiwashukuru na kuwapongeza mawakili wa Serikali kwa kushiriki na kupata mafunzo kwa kuwa, bila mawakili hao kuwepo mafunzo hayo yasingefanyika.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya OWMS pamoja na Mawakili wa Serikali kutoka wizara, taasisi, idara, mikoa na halmashauri nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi Mary Makondo (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo kwa mawakili hao yaliyofanyika jijini Dodoma.

Kwa upande wake, mwakilishi kutoka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA),Elias Nawera amesema kuwa, kupitia mafunzo hayo, mawakili wa Serikali wamepata nafasi ya kujifunza na kuelewa mambo mapya kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika majukumu yao ya kiutumishi. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news