Serikali yawezesha wadau wa michezo kuzalisha vipaji

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI inawawezesha wadau kuwekeza kwenye uzalishaji wa vipaji vya michezo hasa mpira wa miguu kwa kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuweka miongozo mahususi ya uanzishwaji na uendelezaji wa shule maalumu za kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (pichani chini) wakati akijibu swali la Mhe. Norah Waziri Mzeru Mbunge wa Viti Maalumu Juni 19, 2023 Bungeni jijini Dodoma, kuhusu Serikali ina mpango gani wa kuwezesha wadau wa michezo kuwekeza katika kuzalisha vipaji vya Michezo mbalimbali hasa mpira wa miguu.

Mhe. Mwinjuma amesema kuwa, Serikali imeweka mfumo madhubuti wa usajili wa akademia na vituo vya michezo, kupunguza kodi kwenye vifaa vya michezo kama vile nyasi bandia na viambata vyake ili wadau hao wachangie kuendeleza michezo nchini.

Pia Serikali inatoa utaalamu na ushauri katika ujenzi wa miundombinu ya michezo na kuandaa mashindano ya UMITASHUMITA kwa shule za msingi na UMISETA kwa shule za sekondari ili kuwashindanisha, kuibua na kuendeleza vipaji vyao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news