Siku ya Tanzania yafana Uholanzi

NA MWANDISHI WETU

WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi zimeratibu na kuadhimisha Siku ya Tanzania katika Falme za Uholanzi, Mjini The Hague.

Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika Juni 24, 2023 yalikuwa na lengo la kutangaza Utamaduni wa Tanzania nchini humo ikiwa ni sehemu ya utekekezaji wa mkakati wa Wizara kuutangaza Utamaduni na Lugha ya Kiswahili Kimataifa.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Balozi Caroline Chipeta aliwashukuru viongozi wa wizara hiyo kwa dhamira yao ya dhati ya kuutangaza Utamaduni wa Tanzania duniani pamoja na kubidhaisha urithi wa utamaduni kupitia utalii.

"Naipongeza sana wizara kwa juhudi zake za kubidhaisha lugha ya Kiswahili ambapo hapa Uholanzi wadau wengi wanajifunza kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia Chuo Kikuu cha Leiden," amesema Mhe. Caroline.

Kwa upande wake Prof. Mutembei ambaye amehudhuria maadhimisho hayo amepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuhakikisha Utamaduni na Lugha ya Kiswahili zinakuwa moja ya nyenzo muhimu zinazochangia ustawi wa maendeleo ya kiuchumi kwa watanzania.

Maonesho hayo yamejumuisha Urithi wa Utamaduni ikiwemo Vyakula , Mavazi burudani za ngoma, muziki wa Kitanzania ulioongozwa na kikundi Cha Wanne Star pamoja na sarakasi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news