Spika Dkt.Tulia aelekea nchini Morocco

NA DIRAMAKINI

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameondoka nchini leo tarehe 12 Juni, 2023 kuelekea Marrakesh, nchini Morocco.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Kibunge wa Majadiliano kuhusu Dini mbalimbali (Conference on Interfaith Dialogue) utakaofanyika nchini humo Juni 13 - 15, 2023.
Aidha, katika Mkutano huo ameambatana na Waheshimiwa Wabunge Mhe. Dkt. Joseph Mhagama, Mhe. Elibariki Kingu,  Mhe. Esther Matiko pamoja na Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa Mwihambi ndc.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news