TanTrade, Ubalozi wa Misri kuandaa Mikutano ya B2B

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bi. Latifa Khamis leo Juni 20, 2023 katika ofisi za TanTrade amekutana na Maafisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini ukiongozwa na Ndugu Mohammad Ally Atteya na Bi. Leila Adel, ambapo wamezungumzia maandalizi ya Maonesho na Mikutano ya B2B katika sekta ya Hotel na Vifaa vya nyumbani kutoka Misri.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 17-19 Julai, 2023, Zanzibar ambapo Kampuni takribani 15 za Misri kwenye Sekta ya Utalii zitashiriki.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis amesema TanTrade itashirikiana na Ubalozi wa Misri katika uratibu kwa kutoa wataalam kutoka TanTrade Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano huo.

Katika Mkutano huo kutakuwa na Maonesho madogo ya Bidhaa pamoja na mikutano baina ya wafanyabiashara (B2B) wa Tanzania Misri.

Pamoja na kuwahakikishia ushirikiano, Mkurugenzi Mkuu aliwakaribisha kutembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28 Juni -13 July, 2023 katika Uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news