Tanzania, Urusi zakubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan katika ofisi za wizara jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara jijini Dodoma kwa mazungumzo.

Katika mazungumzo hayo ya Mei 31, 2023 viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kihistoria na kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Urusi pamoja na sekta za ushirikiano zilizo katika hatua mbalimbali kwa maslahi ya pande zote mbili.

Vilevile, katika mazungumzo hayo wamejadili juu ya mkutano wa Urusi – Afrika na Kongamano la Uchumi litakalofanyika mwezi Julai 2023 nchini Urusi. Kongamano hilo linatarajiwa kutoa mtazamo wa uhusiano kati ya Urusi na na nchi za Afrika.Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urusi zinashirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi, afya, biashara, viwanda, uwekezaji na utalii ambapo kwa pamoja zimekubaliana kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta tija katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news