Serikali yasisitiza thamani ya miliki bunifu nchini

NA ELEUTERI MANGI-WUSM 

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amefanya kikao na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miliki Bunifu la Kikanda Afrika (ARIPO), Bi. Flora Mpanju tarehe 31 Mei, 2023 katika ofisi za wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. 
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (kulia) akiongea na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miliki Bunifu la Kikanda Afrika (ARIPO), Bi. Flora Mpanju (katikati) Mei 31, 2023 katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Bi.Doreen Sinare.

Bw. Yakubu amesema kuwa, Tanzania inathamini na itaendelea kushirikiana na ARIPO katika sekta ya miliki bunifu ambayo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miliki bunifu Afrika (ARIPO), Bi. Flora Mpanju amesema shirika hilo linathamini sana mchango wa Tanzania katika kazi zao kwa kuzingatia sifa nzuri na uaminifu katika shirika hilo iliyojengwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. 

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Bi. Doreen Sinare pamoja na watendaji wa taasisi hiyo ambapo amesisitiza kuwa COSOTA imeshatoa tangazo la Kampuni Ukusanyaji na Ugawaji Mirabaha ili kuboresha mazingira ya wasanii kunufaika na kazi zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news