Wanasimba msimu ujao hatutakuwa wanyonge-Try Again

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Salim Abdallah (Try Again) amewathibitishia wafuasi wa klabu hiyo kuwa,msimu ujao wa ligi hawatakuwa wanyonge kwani wamejipanga kusuka kikosi imara kwa ajili ya kushinda mataji.
Try Again amesema watasuka kikosi imara kwa ajili ya kuhakikisha wanashinda mataji baada ya kuyakosa kwa miaka miwili.

“Naomba niwahakikishie Wanasimba wote kuwa msimu ujao hatutakuwa wanyonge, tutakuwa imara kuliko ilivyokuwa awali.Tunajua kwa misimu miwili hatukuwa na furaha, lakini msimu ujao tutakuwa bora kwa kuwa tutasajili kikosi imara,”amesema Try Again.
Tayari, wenkundu hao wa Msimbazi wenye maskani yake jijini Dar es Salaam wameingi mkataba na Kampuni ya Sunderland wa udhamini wa jezi na klabu ya Simba wenye thamani ya shilingi bilioni mbili kwa muda wa miaka miwili.

Kampuni ya Sunderland inachukua nafasi ya Vunja Bei ambayo imemaliza mkataba wake wa miaka miwili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news