Waziri Dkt.Chana azuru kambi ya Yanga SC jijini Algers

NA SHAMIMU NYAKI 

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Juni 2, 2023 amewasili katika Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Algers nchini Algeria na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo , Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu ikiwa ni maandalizi ya kushuhudia mchezo wa Fainali ya Pili ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Dar es Salaam Young Africa (Yanga) na USM Alger ya nchini humo utakaochezwa Juni 3, 2023 majira ya saa 2: 00 usiku ambazo ni saa za nchi hiyo.
Mara baada ya kuwasili katika Ubalozi huo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesaini Kitabu cha wageni pamoja na kuzungumza na Balozi wa Tanzania nchini humo pamoja na kupata nafasi ya kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Yanga katika Kambi yao, ambapo mbali na kuwatakia heri, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. ameahidi zawadi zaidi endapo watabeba Kombe na Watanzania wanawaombea na kuwatakia heri pia.
Katika ziara hiyo Mhe. Chana ameambata na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid, Mwenyekiti UWT Taifa Mhe. Mary Chatanda, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ndg. Nicholas Mkapa, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Wallace Karia, baadhi ya Waheshimiwa Wabunge na mashabiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news