Zuio la Rais Dkt.Samia kuuza chakula nje, Mwinjilisti Temba ashauri

NA DIRAMAKINI

MWINJILISTI wa Kimataifa, Alphonce Temba amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo ya kusitishwa uuzaji wa vyakula nje huku akitoa ushauri ili kuweza kuondoa changamoto ambayo imejitokeza baada ya aagizo la Rais.
 
Hivi karibuni Rais Dkt.Samia akiwa ziarani mkoani Mwanza amewataka Watanzania kutumia vizuri chakula, huku wakijihadhari na njaa inayoweza kuikumba Dunia kutokana na sababu kadhaa, ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, athari za UVIKO-19 na vita kati ya Urusi na Ukraine.

Alitoa tahadhari hiyo wakati wa hotuba yake ya kuzindua tamasha la utamaduni na ngoma za asili za jamii ya Wasukuma, zinazochezwa kipindi cha mavuno maarufu kama Bulabo katika viwanja vya Red Cross, eneo la Kisesa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia alisema kutokana na tishio hilo la njaa na mfumuko wa bei duniani, Serikali inakamilisha mchakato wa kununua na kuhifadhi chakula cha kutosha katika maghala ya Taifa kwa tahadhari, lengo likiwa ni kuwahakikishia Watanzania uwepo wa chakula.

Pia aliwasihi wakulima kutouza nje ya nchi mavuno yao,alisema kwa kawaida, mfumuko wa bei katika kipindi kama hiki huwa inatarajiwa kuwa asilimia tano, lakini kutokana na athari za UVIKO-19, vita vya Urusi na Ukraine na mabadiliko ya tabianchi, mfumuko wa bei duniani umefikia zaidi ya asilimia 10 kinyume cha matarajio.

Akizungumzia kuhusu maagizo ya Rais Dkt.Samia, Mwinjilisti Temba amefafanua kuwa, "Ushauri wangu juu ya kauli ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuzuia vyakula kuuzwa nje ya nchi. Awali ya yote nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kujali wananchi wake.

"Mimi binafsi ningetoa ushauri kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 18 na kumuomba Mheshimiwa Rais kuona namna bora ya kuhakikisha biashara za mazao zinaendelea kufanyika ndani na nje ya nchi.

"Nilikuwa nafiki Mheshimiwa Rais angeshauriwa kwamba kama nchi yetu haina vita wala tetesi ya vita na nchi nyingine wala tatizo la kidiplomasia na kumekuwa na biashara zinafanyika withn East Africa.

"Na hili ndilo lengo la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kufungua mipaka na mataifa kwenda kwenye coin moja, viongozi wetu wa Afrika Mashariki wamekuwa wakikutana na kufanya vikao na ushirikiano mkubwa.

"Na faida yake ndio hii uuzwaji wa bidhaa na biashara kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine ili kusiwe na visasi vya nchi kufunga mipaka tulisikia Zambia walifunga sasa Tanzania wanafunga.

"Sasa hoja yangu kubwa ni kwamba, nilikuwa napenda kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba Rais katoka kutoa kauli hadharani kwamba shehena yoyote isiende nje, kuna watu ni binadamu wenzetu kutoka nje, tumefanya nao biashara kwa muda mrefu wanaumia sana.

"Kwa hiyo kauli ya Mheshimiwa Rais ni kubwa na inawezekana rushwa ikatembea pakubwa sana. Inawezekana watu wakaathirika watu wakafilisika, watu wakapata strock wakafa.

"Kwa kuwa watu wamekuwa wakifanya biashara kwa kuruhusiwa ikawa ni haki na watu wamefunga mashehena wamechukua mikopo mabenki huko kwao iwe ni Zambia, Kenya, Uganda iwe Sudan wamekopa mabilioni ya pesa wamekuja huku wana malori wanasafirisha mizigo yao iwe kutoka nje au wanapita Tanzania kwenda kwao halafu inafika hatua kama hiyo.

"Basi Mheshimiwa Rais anapaswa kusema hivi natoa siku saba, natoa wiki moja au natoa siku 14 hakutakuwa tena na shehena yoyote itakayokwenda nje ya nchi kwa sababu hao watu wanatoka nje ya nchi kuja kununua kwa fedha zao na wameshakabidhiwa mzigo wao na wako njiani kwenda Kenya, Uganda au Sudan au mataifa mengine.

"Na tayari wameshanunua wanafika mpakani wanakutana na kizuizi kwamba mizigo hairuhusiwi kutoka watu hawa wanaumia, watu hawa wanafanyaje, watu hawa ni wageni.

"Na stamp zao za siku tatu ni za wiki moja zina expire mtu huyu anarudi nchini kufanya biashara je? Mtu huyu tumemwangaliaje ambaye ni mtu tunamtamani tumekuwa tukisema Tanzania tuna bandari tuna wageni kutoka mataifa mbalimbali wanaweza kuitumia.

"Je? Kwa mantiki hii na dhana hii bandari yetu itapiga hatua kweli. Tunaona watu kule Kariakoo, wafanyabiashara wakipiga kelele kwamba wageni wanakataa kuja, wageni wa kibiashara mara nyingi huwa wanakumbatiwa, wanabembelezwa.

"Wageni wa kigeni wanahitajiwa, tunahitaji tupate watu wa kumshauri Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Rais ana watu wa aina mbili, kuna watu wa kumsaidia Mheshimiwa Rais na watu wa kumshauri Rais hao ni watu wa aina mbili tofauti.

"Na kama Mheshimiwa Rais atapata watu wa kumshauri ambao ni watu watakaomsaidia kushinda katika uchaguzi itakuwa ni kosa kubwa sana kwa sababu hawa ni watu wawili tofauti.

"Kwa sababu mtu huyu anauwezo wa kubadilika katika jambo, hivyo anavyosimama na Mheshimiwa Rais anashinda kwa urahisi, lakini utambuzi yakinifu wa kuona mbali hana sio gifted kwa ajili ya ushauri.

"Kwa ushauri wangu sasa hivi ukienda kule Horohoro, Tarakea, haya malori yalivyojaa yanaleta shida, yanaleta chuki huzuni. Mimi nafikiri the grace period must be given kabla ya agizo la Mheshimiwa Rais halijafanyiwa kazi.

"Isiwe kama mvua, hata mvua ina dalili zake jamani mawingu utayaona, upepo utauona uta escape so haya mambo makubwa makubwa hasa mipaka mtu anafanya biashara amewekeza fedha na hawa ni binadamu ni kama Watanzania manung'uniko yao hayaleti baraka mbele zetu.

"Nafikiri kwamba mipaka isifungwe ghafla unless kuna vita au hatari fulani na hata kama ni vita inaweza kuwa imefungwa shehena inaruhusiwa kibinadamu tunaona huko Ethiopia kwenyewe kuna migogoro, lakini bado shehena ya vyakula inaruhusiwa na wapiganaji wanayaheshimu.

"Mimi nasema haya kwa sababu ya wafanyabiashara na wengine Watanzania ambao wamewekeza fedha zao wamechukua fedha benki, wanakuta ghafla mzigo hauendi na una oda, kwa hiyo tunazua matatizo makubwa kwa wananchi hii ni kero, hii ni shida inahitaji ufumbuzi,"amefafanua kwa kina Mwinjilisti Temba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news