Naibu Waziri Mwinjuma ashuhudia Tanzania ikiitwanga Eritrea vikapu 69-34

NA BROWN JONAS

NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ameshuhudia Timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (Tanzanite) ikiibuka na ushindi wa vikapu 69-34 vya Timu ya Taifa ya Eritrea.
Mchezo huo wa ufunguzi wa kufuzu mashindano ya mpira wa kikapu Afrika umechezwa Juni 17, 2023 katika Uwanja wa ndani wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo ya kanda ya tano yanashirikisha nchi tano ambazo ni Tanzania, Burundi, Rwanda, Sudani ya Kusini na Eritrea, ambapo timu mbili ndizo zitakazofuzu kushiriki mashindano ya Afrika yatakayofanyika mwezi Julai 2023 Nchini Angola.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news