Dkt.Mabula atekeleza ahadi Shibula

MWANZA-Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Mheshimiwa Dkt.Angeline Mabula ametekeleza ahadi yake ya ujenzi wa barabara za mitaa ya Kata ya Shibula aliyoitoa kwa wananchi wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero na kuhamasisha maendeleo jimboni.

Akizungumza wakati wa utekelezaji wa ahadi hiyo, Mratibu wa Mbunge Sekta ya Miundombinu, Mpunzi Mbegeje Kasubi amesema kuwa, Mbunge Dkt.Angeline Mabula ametenga kiasi cha shilingi milioni sita kutoka katika mfuko wake binafsi kwa ajili ya kukodi greda litakalotumika kujenga barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita 10.1 ikijumuisha barabara ya kutoka Bogolanya kuelekea Igogwe kilomita moja.

Pia,Igombe Saccos kuelekea Kisundi kilomita tatu na Butindo kuelekea Kilabela kilomita nne na ya kutoka Shibula Senta kuelekea Butindo.

Aidha, amewapongeza wananchi wa Kata ya Shibula kwa utayari wao na wenyeviti wa Serikali za mitaa ya kata hiyo kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Ofisi ya Mbunge katika kutatua kero za wananchi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Shibula,Leonard Moshi mbali na kumshukuru Mbunge Dkt.Angeline Mabula kwa kutekeleza ombi lao la ujenzi wa barabara korofi ndani ya kata yao, amewapongeza wananchi wake kwa kukubali kutoa maeneo yao yaliyopitiwa na barabara bila kudai fidia na posho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news