Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi leo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Maulid Shaib Ahmada kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Rais, Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

Kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais katika nafasi hiyo, ndugu Maulid alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu,Utawala na Mipango katika Tume ya Utumishi Serikalini, Zanzibar.Aidha, kupitia taarifa hiyo imefafanua kuwa, uteuzi huo wa ndugu Maulid unaanza leo Julai 21, 2023

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news